Mix

Watu 32 wamefariki kwenye maporomoko ya ardhi

on

4
Watu  32 wamefariki katika maporomoko ya ardhi(landslide) katika mkoa wa Hiroshima nchini Japan.Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa saa 24 kuamkia Jumatano asubuhi zikiwa sawa na kipimo cha mvua za mwezi mzima imesema mamlaka ya hali ya hewa ya Japan.

Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha nyumba zikiwa zimefukiwa katika matope na miamba wakati kikosi cha uokoaji kikielekea kwenye nyumba  hizo.Watu wengine tisa bado hawajulikani walipo na afisa mwingine wa serikali ya mtaa katika mji huo amesema “baadhi ya watu wamechukuliwa na maji na ilikuwa vigumu kujua kwa uhakika idadi yao”.Mwandishi wa habari wa BBC ameripoti kuwa kati ya waliofariki wengi ni watoto.1

2

3

 

 

5

Tupia Comments