Michezo

Goli la Mata limeingia katika list ya magoli yaliyofungwa baada ya kupigwa pasi nyingi, linashika nafasi ya ngapi?

on

Staili ya mchezo wa kushambulia ya klabu ya Manchester United imekuwa ikishambuliwa na wachambuzi wa michezo msimu huu lakini hakukuwa na mashaka juu ya ubora wa pasi 45 zilizopigwa kabla ya kufungwa kwa goli la tatu dhidi ya Southampton.
Goli hilo Juan Mata lilihakikishia United ushindi muhimu lakini pia limewezq kuingia katika listi ya magoli yaliyofungwa baada ya kupigwa kwa pasi nyingi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita ndani ya Barclays Premier League.
Kabla ya kufungwa kwa goli hilo Manchester United walipiga pasi 45, na hivyo kulifanya goli hilo kushika nafasi ya pili kwa idadi ya pasi kabla ya goli huku nafasi ya kwanza ikishikwa na goli la Nacer Chadli wa Tottenham aliyefunga goli dhidi ya QPR baada ya kupigwa kwa pasi 48.

Chadli alifunga goli hilo katika mechi ya raundi ya kwanza ya EPL msimu uliopita.

 Listi ya magoli ya magoli yaliyofungwa baada ya namba kubwa ya pasi katika EPL
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Tupia Comments