Mix

‘Nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu’:-Mama Janeth Magufuli

on

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo November  11  2016 baada ya afya yake kuimarika.

2

Mama Janeth Magufuli

Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara‘.;-Mama Janeth Magufuli

‘Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu’ amesema Mama Janeth Magufuli.

Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi November 09 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIVYOMTEMBELEA MKEWE HOSPITALINI MUHIMBILI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments