Wakati kikao cha Bunge kikiendelea leo Dodoma, Mbunge wa Ubungo John Mnyika alitaka kujadiliwe jambo la dharura kuhusu zoezi la uandikishwaji la wapiga kura.
“Mpaka sasa tunavyozungumza zoezi la uandikishaji halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe na Watanzania nchi nzima wako kwenye sintofahamu, lini hasa wataandikishwa kabla ya kura ya maoni ya katiba mpya, jambo hili ni la dharura kwasababu ilikwisha tolewa hoja ya dahraura juu ya jambo hili kwenye mkutano uliopita wa Bunge, ukaagiza kamati ya Bunge ishughulikie na majibu yatolewe kwenye mkutano huu wa Bunge sasa leo mkutano unafungwa bila majibu kutolewa tusitishe shughuli zote tuhakikishe majibu yanatolewa leo“
“Katika mkutano huu nimeomba muongozo juu ya jambo hili mara mbili na mara zote Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu naamini umeipa maelekezo ya kutoa majibu lakini inakwepa kutoa majibu.
Katika mazingira kama haya hakuna sababu yoyote ya kuendelea na mjadala wowote mwingine kwenye kikao hiki cha Bunge, wala kusubiria chochote tupate majibu kwenye mkutano huu wa Bunge ili tuweze kufanya kazi ya kuishauri na kuisimamia Serikali, Waziri Mkuu yuko hapa anaweza kutoa majibu hapa na tukajadili hapa“–Mbunge John Mnyika.
Lakini Spika Makinda akasema hoja hiyo inafanana na hoja ambayo ilitangulia hivyo haiwezi kujadiliwa, kitu ambacho kilisababisha mvutano wa Wabunge.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza taarifa hiyo …
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook