Habari za Mastaa

MGM wanaileta Filamu inayohusu maisha ya Aretha Franklin itayochezwa na Jennifer Hudson

on

Ni miezi saba imepita tokea Malkia wa muziki wa Soul na R&B Aretha Franklin afariki, inaripotiwa kuwa kwa sasa imeandaliwa filamu fupi ya maisha yake inayoitwa ‘Respect’ ambayo itazungumzia maisha yake na imetajwa kutoka rasmi August 2020 chini ya kampuni ya filamu Metro Goldwyn Mayer(MGM).

Mwimbaji Jennifer Hudson ndio ametajwa kuvaa uhusika wa marehemu Aretha Franklin katika filamu hiyo. Inaelezwa kuwa filamu hiyo “Respect” itagusa maisha ya Marehemu Aretha kuanzia utoto, kuanza kuimba kwenye kwaya ya Baba yake ambaye alikuwa mchungaji hadi kuingia rasmi kwenye muziki na kuwa maarufu.

Aretha Franklin alifariki dunia August 16, 2018 akiwa na umri wa miaka 76 mara baada ya kupambana kwa muda mrefu na ugonjwa wa saratani ya kongosho huku akiwa ameaacha vibao vikali ambavyo vilimpatia umaarufu ikiwemo Respect, I say a Little prayer, Think na nyingine nyingi.

VIDEO: Irene Uwoya kaamua kuweka wazi siri za urembo wa ngozi yake

Soma na hizi

Tupia Comments