Premier Bet SwahiliFlix Ad Vodacom Ad

AyoTV

Rais mstaafu Jakaya Kikwete alivyotembelea sehemu anayonunua nguo(+video)

on

Tunayo story kutokea kwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ambapo ametembelea kiwanda cha Binti Africa ambacho kinatengeneza mashati na batiki ambazo amekuwa akizivaa tangu mwaka 2013.

Mstaafu Kikwete amesema kuwa amefika kiwandani hapo ili kuangalia sehemu ambapo nguo anazovaa zinapotengenezwa, amesema badala ya watu kulalamika hakuna maisha bora wanapaswa kujikita kuwa wabunifu.

“Nilikuwa navaa nguo zake muda mrefu ambapo sasa naona viwango vimeongezeka, inaitwa kujiongeza hivyo nampongeza Binti Africa, dada yake na mama yake ambaye amemrithisha ushonaji,”amesema.

MTANZANIA ANAYEWAVALISHA MARAIS, ALIANZA NA MTAJI WA ELFU 40

Soma na hizi

Tupia Comments