AyoTV

Mafuriko yalivyokata mawasiliano Morogoro na Dodoma, wananchi wapewa tahadhari (+video)

on

Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha kukatika mita 14 kwa daraja la Mkundi lililopo kata ya Dumila Wilayani Kilosa hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya mkoa wa Dodoma na Morogoro.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Kebwe amesema kutokana na jambo hilo kuwa la dharura wameunganisha nguvu ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa haraka.

Kebwe amesema hatua ya kwanza waliyochukua ni kurekebisha sehemu iliyokatika kwa kuweka mawe, ambapo wanashirikiana na TANROADS.

“Tunatoa tahadhari wananchi wasijaribu kuvuka kwa kipindi hiki, wakijaribu kufanya hivyo kuna askari tumewaweka kwa ajili ya kuwazuia ili wasisombwe na maji,”amesema.

UHABA WA SAMAKI: WAVUVI WATISHWA NA DORIA YA LESENI “WALIGOMA”

Soma na hizi

Tupia Comments