Mix

Unadhani tatizo la ajira liko Bongo pekeake? Jamaa ana degree yake mwaka wa 13 Uingereza

on

Need-WorkTatizo la ajira ni kilio cha vijana wengi TZ, watu wanalalamika kwamba wamesoma lakini hawajaajiriwa.. unadhani hili liko BONGO pekeake?

Jamaa mmoja Uingereza, Huw Davies ana degree ambayo ameipata mwaka 2002 baada ya kusoma Chuo cha Glamorgan, lakini toka amemaliza mpaka leo hii amekuwa anatafuta kazi.. ni kwamba hajaajiriwa mpaka leo.

JS60477554JPG (1)

Huw Davies

Jamaa huyo mwenye degree ya Geography amekuwa akitafuta kazi inayoendana na taaluma yake  ya masuala ya mazingira kwa miaka 13, ambapo mpaka sasa ameshaomba kazi mara 500, lakini hajawahi kuitwa kwenye Interview hata mara moja.

mer-grants

Mtaa anaoishi Huw Davies

Davies hajataka kufanya kazi nje ya Uingereza, bado ana imani kwamba atapata kazi tu siku yoyote.. kwa sasa anasema yuko tayari kufanya kazi yoyote hata ya kuendesha taxi.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments