Top Stories

Joe Biden atarajiwa kufanya uteuzi Mawaziri

on

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atafanya uteuzi wa kwanza wa Baraza la Mawaziri Jumanne wiki hii, kulingana na taarifa iliyotolewa na Mkuu wake wa Utumishi.

Rais Donald Trump ameendelea na madai yake ya kuwepo na udanganyifu katika uchaguzi wa Rais na kuongezeka kwa upinzani ndani ya chama chake mwenyewe huku akikataa kukubali kushindwa.

Biden ameendelea na maandalizi ya kuchukua madaraka ifikapo Januari 20, licha ya jaribio la Trump la kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Novemba 3.

Trump amepata pigo jingine baada ya kesi yake ya kupinga matokeo kutupiliwa mbali. Hii ni baada ya timu ya kampeni ya Trump kuwasilisha kesi mahakamani iliyonuia kupinga matokeo ya kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika jimbo la Pennsylvania.

TANZANIA YAANZA VIZURI MASHINDANO YA CECAFA,YAWACHAPA DJIBOUTI MABAO 6-0

Soma na hizi

Tupia Comments