Mfalme wa Morocco Mohammed wa VI amepokea simu kutoka kwa Rais wa Marekani Joseph Biden na kumpa pole kwa janga lililotokea nchini Morocco na tetemeko la ardhi.
Katika mawasiliano hayo ya njia ya simu Rais Biden ametoa salamu zake za rambirambi na kueleza dhamira ya Marekani kuwa tayari kutoa misaada muhimu kwa waathirika nchini humo.
Biden akaeleza kuwa Marekani sio tu iko tayari kutoa msaada bali itatoa msaada kulingana na matakwa na mahitaji ya serikali ya Morocco ambapo tetemeko hilo limeua maelfu ya watu na wengine kuwaacha hawana makazi.