Habari za Mastaa

Joh Makini kathibitisha kufanyika kwa video 3 ikiwemo ya Rapper AKA wa South Africa

on

.

.

Good news ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa Joh Makini na G Nako ambao wapo Afrika Kusini Johannesburg kwenye maandalizi ya video zao.

Joh Makini akiamplify kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM Agosti 25 alithibitisha  kufanyika kwa video 3 ikiwemo yake na rapper A.K.A wa South Africa.

‘Kila kitu kimeenda sawa, kila kitu kimeenda jinsi tulivyopanga namshukuru Mungu kwa maana yeye ndio amefanikisha sisi tuweze kufanikiwa ku shoot video za single zenu kwa takribani siku tatu  ukichukulia kama wiki tuko huku Johannesburg na tayari tumeshafanya video tatu   kwa hiyo watu wakae tayari kwa ujio wa G Nako na Joh Makini’ – Joh Makini

.

.

Kuna video ambayo mimi na rapper AKA wa South Africa halafu kuna video ya  G Nako pekee yake ambayo inaitwa Original na kuna video nyingine ambayo mimi nimeshirikishwa na binti mmoja mwimbaji kutokea Tanzania ambaye naye anakuja kwa hiyo vitu vingi vikubwa vinakuja kama nilivyokuambia tupo katika vibe ya kimataifa zaidi na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kila kitu kinaenda sawa dua zetu muhimu katika kuipeperusha Bendera ya Tanzania’ – Joh Makini.

Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Joh Makini

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments