Habari za Mastaa

Ujumbe wa Jokate kwa Idris Sultan baada ya kuchaguliwa kuhost tuzo Uganda

on

Jokate Mwegelo amekuwa na mwaka mzuri upande wa biashara zake huku brand yake ya kidoti ikizidi kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania. Leo Dec6,2016 ameamua kuonyesha jinsi gani amefurahi kuona Idris Sultan anatambulika vizuri nje ya Tanzania ilihali sio mwanamuziki.

Imezoeleka kuonekana mara nyingi wasanii wa muziki ndio wanatambulika na kupewa heshima nje ya Tanzania tofauti na kwa Idris ambaye ni mtangazaji wa redio na mchekeshaji. Idris Sultan amechaguliwa ku host tuzo za fashion  za ASFA huko Uganda Dec9, 2016.

>> ‘Kwa mara ya kwanza mtu ambaye sio msanii wa mziki anaheshimika kimataifa. Tangu siku ya kwanza umetudhihirishia kuwa staa, umekuwa na juhudi katika safari yako, Naiona dunia ‘Hollywood’ inakuita. Wewe bado ni mdogo na bado una nafasi, Itumie vizuri. Ni kawaida kufanya makosa,unaboa wakati mwingine lakini kama binadamu kazi yetu ni kuinuana zaidi ya kubomoa. Hivyo nakutakia kheri ndugu @idrissultan. Mungu aendelee kukuongoza’  -Jokate

Video:’Mimi nilikuwa mwanafunzi ninayepigwa mno darasani’-Idriss Sultan

Soma na hizi

Tupia Comments