Habari za Mastaa

JoJo anaileta kwetu single yake ya pili kwa mwaka huu; ‘Say Love’ na video yake imenifikia! – (Video)

on

Baada ya kupotea kwa miaka 9 kwenye headlines za burudani, msanii wa muziki wa R&B Marekani, JoJo alirudi kuichukua nafasi yake kwa kuzindua video mpya iliyopewa jina  “When Love Hurts” mwezi uliyopita… JoJo karudi tena, na time hii anaileta kwetu video ya single yake mpya, ‘Say Love’.

JOJO3

JoJo aliuambia mtandao wa BuzzFeed kuwa alitaka single hii iwe ya miondoko ya slow jam kidogo kwa sababu hapo awali alitoka kuzindua single ambayo imechangamka sana… >>> “wimbo huu niliamua niufanye uwe slow kidogo, wenye hisia… natumaini watu wataupenda kwa sababu mimi binafsi naupenda naona umekaa poa sana na nina hamu kweli muione video yake…” <<< JoJo.

Kwa sasa JoJo bado yupo studio anakamilisha Album yake ya tatu, iliyopewa jina The High Road itakayoachiwa chini ya Atlantic Records na hii itakuwa album yake ya kwanza toka mwaka 2006!

JOJO

Kama bado hujafanikiwa kukutana na video mpya ya JoJo, nimekusogezea video hiyo hapa chini, bonyeza play kuitazama.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments