Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amepokea vifaa vya msaada kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Njiti) kutoka katika foundation ya Doris Mollel aliyewahi kuwa Miss Ilala.
Msaada huo aliopokea Jokate Mwegelo wenye thamani ya TSh milioni 20 ni pamoja na mashine, vitanda na vifaa mbali mbali vitakavyoweza kuwasaidia watoto Njiti watakao zaliwa katika hospitali za Kisarawe.
Baada ya kupokea msaada wa vifaa hivyo DC Jokate pamoja na Doris Mollel walizungumza ambapo kwa upande wa Doris alielezea jinsi alivyoguswa na ombi la Jokate na kuamua kusaidia katika wilaya hiyo.
..>>>“Tumemkabidhi DC Jokate vifaa vyenye thamani ya Sh M 20, Tayari kusadia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hawaendi hospitali nyingine za mbali kutafuta huduma kwahiyo tunaokoa zile gharama na kwa mkoa wa Pwani hii inakuwa hospitali ya Pili” – Doris
…>>>“Tunashukuru kwa kuanza hii 2020 vizuri kwa tukio hili la ki historia, alichokifanya Doris leo kuileta hii huduma hapa Kisarawe ni kuisogeza hii huduma karibu na wanachi wa Kisarawe ambapo leo Mwananchi asifike Chanika, asifike Muhimbili na wala asiende Mloganzila lakini ahudumiwe hapa hapa Kwenye wilaya yetu ya Kisarawe” – DC Jokate