Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Jokate Mwegelo amewataka Wafanyabiashara Wilayani humo kutopandisha bei ya vyakula kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
DC Jokate ameyasema hayo leo akiwa Ofisini kwake baada ya kumaliza kikao na Uongozi wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Wilayani Korogwe leo March 23,2023.
Jokate amesema kumekuwa na tabia ya Wafanyabiashara kuficha vyakula ili waweze kuongeza bei kwa kisingizio kwamba vyakula hivyo havipatikani sokoni ambapo amewataka Wafanyabiashara kuacha tabia hiyo kwani kufunga ni njia ya kumkaribia Mungu”Msitumie nafasi hii ya Mwezi Mtukufu kuongeza bei ya vyakula”
DC Jokate pia amesema Korogwe ipo salama na chakula kipo cha kutosha Wilayani humo hivyo Wananchi wasiwe na mashaka juu ya hilo.
Katika hatua nyingine Jokate amewatakia Waislamu wote Wilayani Korogwe na Tanzania kwa ujumla Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.