Kuelekea mchezo wa leo wa kukata na shoka wa ligi ya mabingwa wa ulaya baina ya Man City vs Barcelona, kocha wa timu ya Chelsea amesema kwamba Manchester City inakutana na timu mbovu kabisa ya Barcelona katika miaka ya hivi karibuni, wakati vilabu hivyo viwili vitakapochuana usiku wa leo pale Etihad Stadium ‘Machinjoni’.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid ni mara chache sana amekuwa na maoni chanya linapokuja suala la kuijadili Barcelona, na alipoulizwa kuhusu mchezo wa leo alisema haya:
“Nadhani hiki ndio kikosi kibovu cha Barcelona katika miaka mingi iliyopita, hivyo City wana nafasi ya kushinda,” Meneja huyo wa Chelsea alikiambia kituo cha ITV Sport. “Ni kweli kihistoria, Barcelona wana nafasi, lakini hii Barcelona ya msimu huu haina ubora wa Barca ya miaka ya nyuma.
“Ndio wana Lionel Messi, ni mchezaji mkubwa, na wanao wengine muhimu, lakini hii ndio timu mbovu kuliko zote walizowahi kuwa nazo katika miaka hii,” alimaliza Mourinho.
Manchester City na Barcelona zinachuana leo usiku majira ya saa kwa saa za Afrika Mashariki. Millardayo.com itakuletea matokeo na video za marudio ya mchezo muda mfupi baada ya mchezo kumalizika.