Vituko/ Comedy

Mchekeshaji Joti kaanza na muonekano huu wa nywele kwa mwaka 2015.

on

Joti 1Asilimia kubwa ya mastaa wengi wa duniani huwa wanapenda kutengeneza kitu ambacho kitakua tofauti na wengine ili kumtengenezea utambulisho wake popote anapokuwepo na baadae muonekano wao huigwa na watu mbalimbali, mfano wa hii ni Balotelli.

Ni mitindo mingi ya nywele tumeiona kwa mastaa ukiwemo mtindo wa kiduku ambapo kwa sasa mastaa wengi wananyoa hivyo, kuna wengine wanaachia nywele zinakua nyingi ambapo mtindo huu wengi huuita ‘Mwembe’ kwa wingi wa nywele kichwani.

Sasa sasa hivi staa kutoka kundi la Original Komedi mchekeshaji Joti kaamua kuianza 2015 kwa mtindo huu ambao  hajasema unaitwaje lakini kwenye post zake aliandika >>> ‘Kwaheri 2014 sasa karibu 2015, karibu babaaa…..my new style’

jotii3

jotii1

Tupia Comments