Mix

Tutegemee kuiona Orijino Komedi tena? Hali ya Vengu nayo vipi?

on

Kwako ambaye unawafuatilia mabingwa wa kuchekesha wanaoishikilia rekodi ya Wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV Tanzania Orijino Komedi ambao hawajaonekana kwenye TV kwa muda mrefu sasa na ungependa kusikia chochote.

Ayo TV na millardayo.com zimepiga stori na mmoja wa wachekeshaji wa kundi hilo Joti kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo show ya Orijino Komedi na moja ya maswali aliyojibu ni kuhusu kama itarudi huku pia akituambia hali ya Vengu ambaye ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa.

>>>”Mpango upo kwa sababu wakati tunafanya hii kazi hakuna mtu ambaye alijua kama komedi ingeweza kuja. Hata sisi pia tuna time kwamba tumefanya kazi muda mrefu sana zaidi ya miaka 10, hivyo namna ya kupumzika tunapanga sisi.

“Tunajua mashabiki, tunajua watu wanaotutazama kila siku wanataka wafurahi lakini sisi tunaofanya hiyo kazi ni binadamu pia tunahitaji kupumzika, kuishi na familia, kutengeneza maisha, kutulia kwanza akili zetu kutafuta vitu vingine zaidi.” – Joti.

“Ni kweli…ana nafuu kwa sababu kwa sisi tunaomjua, kumuona na kuishi naye tunajua nafuu yake ikoje. Kwa mtu mwingine anaweza kusema hana nafuu lakini sisi tunasema ana nafuu.” – Joti.

PLAY kwenye hii VIDEO ili kujua kila kitu kuhusu Show hiyo iliyokuwa inaundwa na wachekeshaji Masanja Mkandamizaji; Joti, Wakuvanga, MackReggan aka Shemeji, Mpoki  na Vengu ambaye amekuwa akiugua kwa muda mrefu.

Video:Ujio wa Staa wa India Sanjay Dutt Tanzania kwa siku 21>>>

 

Soma na hizi

Tupia Comments