Habari za Mastaa

Mambo matano ya Alikiba na Baraka Da Prince kuvamiwa na Majambazi South Afrika

on

millardayo.com na AyoTV zilipata taarifa kuhusu waimbaji wa muziki wa bongofleva Alikiba na Baraka Da Prince ambao wote wako chini ya lebo ya Rockstar 4000, kuvamiwa na Majambazi wenye silaha Afrika Kusini saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki July 20 2016.

  1. Management inayowasimamia imeiambia millardayo.com kwamba wawili hawa pamoja na watu wengine wakati wanavamiwa, walikua kwenye eneo kulikofanyika kikao cha maandalizi ya kazi zilizowapeleka Afrika Kusini kwa siku saba.
  2. Majambazi hao walikua sita na walikua pia na silaha za moto (bunduki)
  3. Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo Majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea Bunduki kina Alikiba kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.
  4. Baraka Da Prince na Alikiba wote ni wazima wa afya na hawakurudhika na chochote kwenye hilo tukio
  5. Pamoja na tukio hili kutokea, Baraka na Alikiba hawatosimama kufanya projects zao… wamechukua mapumziko mafupi na kisha wataendelea.

Ali na Baraka

ULIIKOSA HII YA ALIKIBA LIVE KWENYE STAGE ALIPOWAPANDISHA WEMA SEPETU NA JOKATE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

ULIIKOSA HII YA NAJ AKIONGEA KUHUSU TAARIFA ZA UJAUZITO WA BARAKA DA PRINCE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments