Top Stories

JPM “Sipendi vya bure dhamira yangu inanisuta”

on

Rais Magufuli amesema alitumia muda mrefu kufikiria kukubali ombi la kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutokana na Jitihada, anazofanya katika kuiletea maendeleo Tanzania.

Rais Magufuli amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya kukaa kwa muda mrefu ni kile alichokiseMa, ni imani yake ilikuwa ikimsuta juu ya kutopenda vitu vya bure, kama alivyokuwa amefundishwa na Baba yake mzazi pindi alipokuwa mdogo.

“Nilipopewa barua ya kunipa Shahada ya Udaktari nilijiuliza kwa nini mimi, sijawahi kupenda vitu vya kupewa bure, nilikaa mwezi mzima sijaijibu, dhamira yangu ilikuwa inanisuta kwa nini nipewe cha bure, ‘Knowledge’ niliyopewa na Baba ilikuwa inanisuta JPM

Nilikubali kutokana na historia yangu na Mkapa, kingine kimenisukuma kukubali, hizi hazitolewi kwa mtu binafsi ni kwa niaba ya wengi, hii shahada imetolewa kutambua mafanikio yaliyopatikana kwenye miaka 4 ambayo hayajatokana kwa ajili yangu bali Watanzania.” JPM

VIDEO HD: LIPUMBA AFUNGUKA RAIS MAGUFULI KUTUNUKIWA SHAHADA

Soma na hizi

Tupia Comments