AyoTV

Kilichofanya Rais Magufuli aivunje bodi ya TRA (+ video)

on

Ilikua ni kwenye mahafali ya chuo kikuu huria Bungo Kibaha Pwani na Rais Magufuli alialikwa ambapo wakati anaongea mbele ya waliohudhuria aligusia pia kwanini aliivunja bodi ya TRA.

Juzi hapa tumekuta hela BILIONI 26 zilizokua zimetolewa TRA kwa ajili ya matumizi ya TRA zikapelekwa kwenye Mabenki matatu kama Fixed Deposit Account na bodi ikapitisha, ndio maana nilipozipata hizo hela nimezichukua na bodi kwaheri‘ – Rais Magufuli

Pamekua na mchezo huu kwa Ma-chief Executive wengi, zinapotolewa pesa kwa ajili ya miradi flani wao wanazichukua alafu wanaziweka kwenye Benki za kibiashara kwa mazungumzo kati ya huyo mkuu wa Taasisi na Mabenki husika‘ – JPM

Unaweza kumtazama hapa chini Rais Magufuli alivyozungumza..

VIDEO: Agizo jingine la Rais Magufuli kwa Waziri wa elimu.

VIDEO: ‘Amefeli kidato cha sita, kwanini akwepe kurudia? – Profesa Ndalichako

Soma na hizi

Tupia Comments