Mix

President Magufuli kateua mwingine leo January 17 2017

on

Kazi ya millardayo.com na AyoTV ni kukusogezea matukio na habari mbalimbali kila zinapotokea ambapo kwenye post hii ni habari kutoka Ikulu Dar es salaam.

Taarifa ikufikie kwamba President John Pombe Magufuli leo tarehe 17 January, 2017 amemteua Jaji Prof. Ibrahim Juma kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania na hiyo ni kuchukua nafasi ya Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi ya kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania ambapo sasa atakaimu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania mpaka hapo Rais Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Uteuzi wa Prof. Ibrahim Juma unaanza mara moja.

ULIPITWA???? Kuona Makomando wa jeshi la Tanzania wakionyesha uwezo mbele ya Rais Magufuli? bonyeza play kwenye hii video hapa chini ujionee

Soma na hizi

Tupia Comments