Mix

PICHA 6: Rais Magufuli kaondoka Tanzania leo January 28

on

Kazi ya millardayo.com na AyoTV ni kukusogezea matukio yote kiganjani mwako ambapo time hii ninakupasha kwamba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameondoka Tanzania leo January 28.

Safari iliyomuondoa JPM ni ya Addis Ababa Ethiopia ambako anakwenda kuhudhuria mkutano wa kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Picha ya kwanza hapo juu inamuonyesha akisalimiana na Rais wa muungano wa visiwa vya Comoro Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 muda mfupi kabla ya safari kuanza.

Hapa ni Rais Magufuli akiagana na Makamu wa Rais, Waziri mkuu pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Rais Magufuli akisalimiana na Wakuu wa mejeshi kabla ya kwenda kupanda Ndege

President akiwapungia Wafanyakazi uwanja wa ndege

JPM akiagana na Makamu wa Rais, Waziri mkuu Majaliwa na Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa Dar es salaam.

VIDEO: Ulikosa kuona Makomando wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli? tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments