Top Stories

Uteuzi wa Rais Magufuli umegusa wawili leo, mmoja Katavi mwingine Mwanza..

on

Bado Rais Magufuli yuko kwenye mipango ya kuisuka Serikali yake ya awamu ya tano iendelee na kazi aliyoahidi Watanzania, najua kama umekuwa karibu na vyombo vya habari wiki moja iliyopita Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kutokana na tuhuma za kufanya vurugu Kikaoni, nafasi hiyo ilikuwa wazi kuanzia hapo.

January 29 2016 nina mawili ya uteuzi wake, kwanza  Rais Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa.

Kingine ni kwamba Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa Polisi, Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa pia.

Taarifa ya Ikulu imesema sababu ya kuteua Maofisa hao wa Polisi ni kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

MAGUFUULI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments