Stori Kubwa

Rais Magufuli kaamua Bilioni zilizokua zitumike sherehe za uhuru 9 Dec matumizi yake yawe kama ifuatavyo.

on

Kwa sababu tayari Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kwamba sherehe za Uhuru siku ya December 09 2015 hazitokuwepo, ninayo taarifa nyingine kuhusu maamuzi mengine ya pesa ambazo zilitengwa kwa shughuli hiyo.

Taarifa kutoka Ikulu imetolewa kwamba fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kutumika kugharamia sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika December 09 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco iliyopo Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia za barabara za lami.

Taarifa hiyo ya Ikulu imesema tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

Hii hapa taarifa yote ya Ikulu.

IMG-20151130-WA0042

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kubadilisha matumizi ya pesa, kama unakumbuka siku alipolihutubia Bunge November 20 2015 aliagiza zaidi ya Milioni 200 zipelekwe kununulia vitanda vya wagonjwa hospitali ya Muhimbili badala ya kutumika kwenye sherehe za Wabunge Dodoma… kama ulipitwa na hiyo, video yake hii hapa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments