Top Stories

Daraja juu ya Bahari Dar es salaam… Rais Magufuli alivyohakikishiwa ujenzi wake leo.

on

Vichwa vya habari za siasa Tanzania bado vinaendelea kubeba stori kila mara kuhusu Rais Magufuli… inawezekana ni kawaida kabisa kila siku kukutana na habari zaidi ya tatu au nne kuhusu Rais Magufuli tangu siku ya kwanza alipoapishwa na kuanza kazi ya Urais wa Tanzania.

MAGUFULI

Rais Magufuli akionesha ramani ya daraja la Salender, enzi hizo alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Ninayo nyingine kutoka Ikulu sasahivi, hii inahusu Rais Magufuli kumuaga Balozi wa Korea Kusini, Chung IL ambapo Balozi huyo amemhakikishia Rais Magufuli kwamba daraja hilo litajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini.

IMG-20151130-WA0045

Daraja hilo litajengwa kuunganisha eneo la Coco Beach na Ocean Road ambapo litakuwa na urefu wa kilometa 6.3.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments