Mix

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 10 2016

on

Taarifa iliyotolewa leo september 10 2016 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua  Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Wakurugenzi walioteuliwa 
⦁ Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma
⦁ Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
⦁ Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
⦁ Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
⦁ Hudson Stanley Kamoga – Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
⦁ Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
⦁ Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
⦁ Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
⦁ Bakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
⦁ Juma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
⦁ Butamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
⦁ Waziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
⦁ Fatma Omar Latu – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

Wakurugenzi wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wametakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne september 13 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV, SEPTEMBER 10 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments