Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo October 24 2016 amefanya mazungumzo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI.
Ziara ya mfalme huyo ni kuimarisha uhusiano baina ya Morocco na Tanzania, mfalme Mohamed VI akiwa Ikulu Dar es salaam na ujumbe wake wamesaini makubaliano takribani 22 ya ushirikiano katika sekta ya kilimo, gesi, mafuta, reli ya Liganga na Mchuchuma na Sekta ya utalii.
Baada ya kutiliana saini kwa mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Morocco Rais Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na Mfalme Mohamed VI wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa kisasa mkoani Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.
>>>’Mbali na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza mambo mbalimbali na Mfalme Mohamed VI wa Morocco na nimemuomba atujengee Uwanja mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na thamani kati ya dola milioni 80 hadi 100 na amesema ataujenga, kwa hiyo utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam‘.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
UNAWEZA KUANGALIA HII VIDEO KUHUSU MIKATABA TAKRIBANI 22 ILIYOSAINIWA NA TANZANIA NA MOROCCO