Watu mbalimbali wamekua na maoni juu ya utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli akiwemo Mstaafu Mwinyi, Wananchi na hata baadhi ya Wabunge bungeni walisikika wakisema wanatamani Rais huyu atawale kwa muda mrefu.
Leo wakati Rais Magufuli akiwa kwenye ziara yake Tanga amenukuliwa akijibu hicho kinachosemwa kuhusu yeye kuendelea kukaa madarakani hata baada ya muda wake kumalizika.
JPM amesema hawezi kukaa madarakani kwenye Urais kwa miaka 20 kama alivyoombwa pia na Mbunge Steven Ngonyani kwasababu ni kinyume na katiba.
FULL VIDEO ya alichokiongea Rais Magufuli unaweza kutazama kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Yusuf Manji Mahakama kuu tena, bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: JPM awakutanisha Paul Makonda na Ruge Mutahaba, bonyeza play hapa chini kutazama