Agizo la Rais Dr. John Magufuli alilolitoa Mbeya akiwa Chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia la kuwataka TCU ndani ya siku kumi kufika chuoni hapo kuhakikisha suala la ithibati ya programu zilizoombwa na chuo linakamilika chini ya usimamizi wa waziri Prof Joyce Ndalichako, limetekelezwa.
Ndani ya saa 24 tu toka Rais aagize, Waziri Ndalichako amefika chuoni hapo katika campus ya Rukwa akiwa na Watendaji wa TCU ambapo baada ya ukaguzi Waziri alieleza kutoridhika na kasi ya utekelezaji wa jukumu hilo na Tume na kuwataka kubadilika na kufanya kazi kwa kasi ya Serikali ya awamu ya Tano na kama kuna Watumishi wanaoshindwa kuendana na kasi hiyo wajiondoe au waondolewe huku akimtaka Mwenyekiti wa Bodi kusimamia kusimamia hilo bila uoga.