AyoTV

VIDEO: Dakika 20 za Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa mradi wa mwendokasi

on

Leo January 25 2017 President Magufuli amefungua rasmi awamu ya kwanza ya miundombinu na utoaji wa huduma ya usafiri wa haraka wa mabasi (BRT) katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mradi huo Rais Magufuli ameiomba Benki ya Dunia kuharakisha mchakato wa kutoa fedha za mkopo utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Ubungo (Ubungo Interchange) ili kuongeza ufanisi wa mradi. Aidha Rais Magufuli ameyazungumza haya…..

‘Tunataka Dar es Salaam liwe Jiji la kisasa, ndugu zangu wa Dar es Salaam nataka mniamini hivyo, hivi karibuni tunapitia tenda na tutapata Mkandarasi wa kuanza kujenga reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo kuna jumla ya kilometa 200 na treni zitakazopita zitatumia mafuta na umeme’ 

‘Lakini pia mchakato wa kujenga barabara ya haraka (Express Road) kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze yenye njia 6 na hatua zote zimekamilika na kilichobaki ni mazungumzo na wakandarasi kabla ya kuanza kujenga’

Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama

VIDEO: Rais Magufuli alivyosimama na kumtunza Mrisho Mpoto, Bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments