Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao watanaoesha nia kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali kununua korosho kwa bei elekezi ya shilini 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa korosho.
Rais Magufuli “Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima“.
“haiwezi Serikali imepanga bei ya korosho 3300, halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, mkitaka ushuru msimamie vizuri bei ya korosho, siwezi nikakusanya hela mikoa mingine nije niwalipe nyinyi.” Rais Magufuli