AyoTV

Agizo la Magufuli kwa Magereza “Itasaidia kurekebisha wafungwa” (+video)

on

Katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhusu uchumi wa viwanda, Jeshi la Magereza limeingia makubaliano ya kuboresha kiwanda cha viatu vya Ngozi cha Gereza la Karanga Moshi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Injinia Masoud Omary amesema uboreshwaji wa kiwanda hicho unatokana na agizo la Rais Magufuli ambapo amesema malengo ya mpango huo ni kuboresha kiwanda hicho pamoja na ujenzi wa viwanda vipya.

Naye Kamishina Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike amesema kwa upande wao ni faraja kwa sababu hiyo ni fursa kwani wanashughulika na wafungwa ambapo hiyo itasaidia kurekebisha wafungwa pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Mbunge aliyehama CHADEMA kafunguka “Kuna vitu nimeviiba, walituma watu”

Soma na hizi

Tupia Comments