Leo Jeshi la Polisi Tanzania limezungumza na Waandishi wa habari kuhusu mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania kufanya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambapo ndani yake likazungumzia sehemu ya Tanzania inayoongoza kwa Wanawake kupiga Wanaume.
Mpaka mwaka 2016, rekodi inaonyesha kwamba Mkoa ulioongoza kwa Wanawake wake kupiga Waume zao ni Iringa ambapo Msemaji wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema “Iringa iliongoza kwa kuripotiwa Wanaume kupigwa na Wanawake”
Unaambiwa sababu kubwa za Wanawake kupiga Wanaume kwenye Mkoa huo ambao sifa yake nyingine ni usafi wa mji kwa asilimia zote, ni ulevi na wivu wa kimapenzi” Unaweza kutazama zaidi akiongea kwenye hii video hapa chini.
DUNIANI: Mwanamke aliyeolewa na mwana wa Mfalme bila kugundua….. bonyeza play hapa chini kupata uhondo wote
Mwanamke mwenye ndevu alivyoombwa ndevu zake zimtajirishe mtu kishirikina… BONYEZA PLAY HAPA CHINI