Top Stories

Kesi ya Kigogo wa UDART na mkewe, Mahakama yaelezwa ulipofikia Upelelezi (+video)

on

Upande wa Jamhuri katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena na wenzake wanne umedai kuwa upelelezi wa shauri bado haujakamilika.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Ester Martine mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizire kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelelezi bado haujakamilka hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Rwizire aliahirisha kesi hiyo hadi June 24 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washtakiwa wamerudishwa rumande.

Mbali na Kisena washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mkewe Frolencia Membe, Kulwa Kisena, Charles Newe na raia wa China, Cheni Shi.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 19 ikiwemo kusababisha hasara kwa UDART ya Sh. Bilion.2.41.

Katika mashtaka hayo yapo ya Kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, Wizi wa mafuta na utakatishaji fedha wa Sh. Bilioni.1.2, kughushi na kusababisha hasara ya Bilioni.1.4.

MAHAKAMA YAAMURU WEMA SEPETU AKAMATWE

Soma na hizi

Tupia Comments