Michezo

John Terry na mkataba wake na Klabu ya Chelsea…

on

John TerryKlabu ya Chelsea iko katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England msimu huu, fans wana imani kuiona klabu yao ikitwaa taji hilo la ubingwa.

Kiwango cha nahodha wa ChelseaJohn Terry kinahesabiwa pia kwamba ni mchango mkubwa kwenye mafanikio ndani ya klabu hiyo, ninayo story nyingine kuhusu jamaa huyu leo.

Terry amesaini mkataba mpya na klabu yake hiyo na atakuwa akipokea kitita cha pound 150,000 kwa wiki.

Mkataba wa Terry na Klabu yake ya Chelsea utaisha baada ya msimu huu wa 2015-16 kumalizika.

Terry ameichezea Chelsea mechi 661 tokea mwaka 1998 huku akiwa amefunga magoli 63 akiwa kama beki tangu alipocheza mechi yake ya kwanza kabla ya kupata namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza mwaka 2000.

terry

Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho ameutaja mkataba huo kuwa ni sahihi kwake kutokana na uwezo wake anaouonyesha ndani ya klabu.

Nafasi ya kuwa beki wa Chelsea ina record nzuri kwake, anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa beki aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na Chelsea mpaka sasa.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments