Top Stories

Kilichojadiliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA leo, kuja na tamko hili Jumatatu

on

Kesho Jumatatu July 31, 2017 Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kitakutana na  Waandishi wa Habari Dar es Salaam kutoa tamko juu ya maazimio na hutua zitakazochukuliwa na Chama hicho kuhusiana na mambo mbalimbali.

Hatua hiyo inakuja baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo July 29-30, 2017 katika Hotel ya Double Tree, Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema imesema kuwa ajenda ambazo zimejadiliwa ni pamoja na hali ya kisiasa, hali ya uchumi na kukamatwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama hicho.

ULIPITWA? Tundu Lissu afunguka ishu ya kutaka kupimwa mkojo na mengine…play kwenye video hii!

ULIPITWA na hii VIDEO? Alichozungumza Wakili Fatma Karume baada ya Tundu Lissu kupewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu…bonyeza PLAY kutazama!! 

Soma na hizi

Tupia Comments