Michezo

PSG inapata hofu Neymar anaweza kuwakosa Man United

on

Club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kuna uwezekano mkubwa ikamkosa mchezaji wake tegemeo Neymar kutokana na staa huyo kuripotiwa kupata majeraha, Neymar anahofiwa kuumia vibaya katika mchezo wa French Cup dhidi ya Strasbourg uliyomalizika kwa PSG kupata ushindi wa 2-0.

Neymar anahofiwa kuwa ametonesha enka ya mguu wake ambayo mara ya kwanza alivyoumia ilimuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, Neymar kutokana na kuumia huko katika mchezo wa French Cup, Neymar anahofiwa kuwa atakosa game ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Man United katika uwanja wa Old Trafford February 12 na kurudiana March 6.

Katika game hiyo Neymar alicheza kwa dakika 62 na kutolewa kwa kupata majeraha na nafasi yake ikachukuliwa na Moussa Diaby, hilo ni pigo la pili kubwa kwa PSG kwani tayari Marco Verratti  anahofiwa kuwa fiti baada ya kuumia na kutolewa nje katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa dhidi ya Guingamp uliyomalizika kwa PSG kushinda 9-0.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments