Michezo

Zidane sasa anamsubiria Rabiot amalizane na PSG

on

Baada ya mama mzazi wa mchezaji wa Paris Saint Germain Andrien Rabiot kukiri kuwa mwanae yupo PSG kumalizia mkataba wake hadi mwisho wa msimu ili aondoke, kwa madai ya kuwa anateswa PSG na anaonekana kama mfungwa, club ya Real Madrid imeanza kuinyatia saini ya staa huyo.

Real Madrid ambayo ipo chini ya kocha wao mpya Zinedine Zidane inatajwa kuwa imeanza kumuweka katika rada zao Andrien Rabiot, AS wameripoti kuwa Real Madrid na Rabiot wamefikia makubaliano tayari wanasubiri mkataba wake umalizike mwisho wa msimu huu.

Andrien Rabiot mwenye umri wa miaka 23 ameondolewa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha PSG, hajapata nafasi ya kuichezea PSG toka December baada ya kugoma kusaini mkataba mpya katika club hiyo, Zidane alikuwa anataka kumsaini Rabiot toka msimu wa majira ya joto uliopita kabla ya kujiuzulu Real Madrid.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments