Habari za Mastaa

Mwanasheria wa Wilaya Philadelphia atoa tamko kuhusu kesi ya Meek Mill

on

Inaripotiwa kuwa baada ya rapper Meek Mill kuendelea kutumikia kifungo cha nje kwa kuwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka 11 sasa huenda mashtaka yake yakatupiliwa mbali na Meek Mill anaweza kuwa huru.

Inaelezwa kuwa Mwanasheria wa Wilaya mjini Philadelphia Larry Krasner ametoa maamuzi ya Jaji Genece Brinkley kuondolewa kwenye kesi ya rapper huyi ambapo shauri la Meek Mill litarudiwa  kusikilizwa na Jaji mwingine. Inaripotiwa kuwa Brinkley aliwahi kuwa Jaji wa kesi ya Meek Mill mwaka 2008 aliposhtakiwa kwa kujihusisha na madawa ya kulevya pamoja na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Mwanasheria wa Wilaya hiyo ametoa kauli kuwa Jaji Brinkley amekuwa ni mbaguzi kutokana na hukumu ambazo amekuwa akizitoa kwenye kesi hiyo hasa baada ya hukumu ya mwaka 2017 ya kwenda jela miaka 2-4 kwa kuharibu masharti ya muda wa Uangalizi.

NANDY: “SINA NAMBA YA RUBY, MAMA YANGU ANAMPENDA SANA”

Soma na hizi

Tupia Comments