Michezo

Man United hati hati kumpoteza Ander Herrera

on

Club ya Man United huenda ikapata pigo kwa kumpoteza kiungo wake muhimu katika kikosi chao Ander Herrera, taarifa za kuwa staa huyo anaweza akawahama Man United zinazidi kupata kasi kutokana na Ander Herrera kuhusishwa kuwa mbioni kujiunga na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Mkataba wa Ander Herrera na Man United unamalizika June 2019, licha ya Man United kuwa na matumaini ya kumbakiza kikosini Ander Herrera, bado hajasaini mkataba mpya unaweza kusema bado hawajafikia makubaliano, imeripotiwa kuwa Ander Herrera analipwa pound 80000 akiwa Man United hivyo anashinikiza mkataba mpya aongezewe hadi 150000.

Huku vyanzo mbalimbali baadhi yao vikiripoti kuwa Ander Herrera anataka kulipwa pound 200000 kwa wiki, Ander Herrera mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na uhakika wa namba toka Ole Gunnar Solskjaer kuonekana kumuamini zaidi toka amepewa Man United, hivyo wengi hawaamini kama Man United itamuachia kirahisi aende kucheza League 1.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments