Michezo

FIFA yatoa ufafanuzi kuhusu kura za Misri kutotambulika kwa MO Salah

on

Baada ya siku moja kupita toka idaiwe mchezaji wa Liverpool anayeichezea pia timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah kukasirishwa na shirikisho la soka la nchini Misri EFA kwa kutompigia kura katika tuzo za The Best FIFA, kitu ambacho kinadaiwa kutompendeza MO Salah.

Kutokana na kuonekana Salah kutopendezwa kwa kutoona kura ya kocha wake wa timu ya taifa na nahodha wake wakiwa wamemchagua, EFA walituma maombi FIFA kupata ufafanuzi kwa nini kura ya kocha wao na nahodha wao haijaonekana na wao walimpigia kura MO Salah.

FIFA wametoa ufafanuzi kuhusiana na hilo na kusema kuwa kura za Misri hazijahesabiwa kama kura kutokana na kuharibika kwa maana zilipigwa kwa kuandikwa kwa herufi kubwa.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments