Michezo

Lionel Messi anataka kuhamia Ligi Kuu ya Marekani

on

Mshambualiaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika club ya FC Bacrelona ya Hispania Lionel Messi inahisiwa kuwa inawezekana atakapotaka kumaliza soka lake atahama kabisa bara la Ulaya na akaenda kucheza soka nje ya Ulaya.

Tetesi hizo za Lionel Messi kuwa mbioni kwa miaka ya baadae kwenda kucheza Ligi Kuu ya Marekani MLS zimekuja kutokana na kiungo wa Atlanta ya Marekani Pity Martinez kueleza kuwa ameulizwa na Lionel Messi kuhusu Ligi Kuu ya Marekani kauli ambayo imetafsiriwa kama kuanza kwa uchunguzi wa staa huyo.

Kauli hiyo aliiweka wazi Martinezi akihojiwa na TyC Sports“(Messi) ameniuliza kuhusiana na Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kwamba kuna nini kinaendelea” Lionel Messi na Pity Martinez kwa sasa wote wapo pamoja katika kambi ya timu yao ya taifa ya Argentina kwa ajili ya mechi za kimataifa zilizopo katika kalenda ya FIFA.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments