Michezo

Staa wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania kapiga hat-trick leo

on

Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Yussuf Poulsen mwenye asili ya Tanzania anayekipiga katika club ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, leo amefanikiwa kufunga hat-trick katika mchezo wake wa Ligi Kuu nchini Ujerumani wakiwa nyumbani na timu yake ya RB Leipzig dhidi ya Hertha BSC.

Poulsen leo alikuwa sehemu ya kikosi cha RB Leipzig kilichocheza dhidi ya Hertha BSC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 5-0, magoli ya RB Leipzig yalifungwa na Emil Forsberg dakika ya 17 na Yussuf Poulsen aliyefunga magoli matatu (hat-trick) dakika ya 27, 56 na 62 huku goli la mwisho likifungwa na Amadou Haidara dakika ya 64.

Ushindi huo umewafanya Yussuf Poulsen na timu yake waendele kuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kwa kuwa na point 52, Borussia Dortmund wakiongoza kwa kuwa na point 63 wakifuatiwa na FC Bayern wenye point 61, timu zote hizo zilizo nafasi tatu za juu zimecheza jumla ya game 27.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri baba yake mzazi Yussuf mzee Yurary ana asili ya Tanzania kutoka Chumbageni Tanga na alifariki kwa kansa wakati Yussuf akiwa na umri wa miaka 6, mama yake Yussuf ni raia wa DenmarkYussuf Poulsen wengi tumemfahamu hivi karibuni baada ya mafanikio yake Bundesliga.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments