AyoTV

VIDEO: TFF imetangaza idara mpya, Wambura baada ya kuondoka bodi ya Ligi

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa katibu mkuu wake Wilfred Kidao limetangaza kuanzisha idara mpya ya habari na masoko na kuamua kumuajiri aliyekuwa afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura.

TFF imetangaza kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya majadiliano yaliokaa na kamati ya utendaji ya TFF na kuona kuna haja ya kuwepo kwa idara kama hiyo kwenye taasisi kama TF, Wambura anaondoka bodi ya Ligi na kurudi TFF alipowahi kupafanyia kazi kwa miaka kadhaa.

Nafasi ya Wambura bodi ya Ligi itatafutwa mbadala wake kwani hata Wambura alikuwa kamaliza muda wake katika kutumikia nafasi hiyo, bado haijajulikana ni nani atakuwa mbadala wa Wambura katika bodi ya Ligi licha ya majina kadhaa makubwa kuanza kuhusishwa.

AUDIO:CLUB YA AS ROMA YA ITALIA IMEANZA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI

Soma na hizi

Tupia Comments