Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Simon Msuva atuma salamu kwa Rais Magufuli

on

Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva, akihojiwa na AyoTV ametoa salamu za shukrani kwa Rais John Pombe Magufuli baada ya kuonesha kuwa yupo upande wao kwa kutamka kuwa wamejitahidi.

Maneno yalikuwa mengi mitandaoni baada ya Taifa Stars kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Senegal na kufungwa kwa magoli 2-0, hivyo Rais Magufuli aliwapongeza na kusema kuwa wamefungwa magoli mawili wakiwa wanacheza na timu bora.

“Sisi kama wachezaji tumepokea vizurii kwanza tunamshukuru Rais (JPM) ambaye anatupa sapoti kila siku ni muelewa chochote anachosikia kutoka kwetu na anachokiona anakuwa ni muelewa”>>>Msuva

VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia

Soma na hizi

Tupia Comments