Top Stories

Mchungaji awalazimisha Waumini kulamba viatu vyake

on

Leo March 20, 2018 stori ninayokusogezea ni ya Mchungaji mmoja kutoka Nigeria ambae makao yake yapo Afrika Kusini ambapo amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya ku-post picha zake wakati wa kuabudu mitandaoni.

Anafahamika kwa jina ‘Nabii’ Andrew Ejimadu ambae ni msimamizi mkuu wa kanisa la Christ Freedom Ministries alishangaza maelfu ya watu baada ya kupigwa picha zilizoonyesha waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake ili kupata baraka na miujiza.

Nabii huyo ndie aliyeweka picha hizo katika ukurasa wake wa Facebook na kuandika: “Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.” 

“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” – Andre Ejimadu

‘Nabii Shillah anaegawa Pesa’ afunguka chanzo cha utajiri, amtaja TB Joshua, Masanja

 

Soma na hizi

Tupia Comments