Top Stories

VIDEO: “Narudia tena Yanga na Simba Sio wenye CECAFA”-Musonye

on

Michuano ya AFCON 2019 inafikia tamati July 19 2019 kwa mchezo mmoja wa fainali kati ya Algeria dhidi ya Senegal kuchezwa, ila gumzo na wengi walishangazwa baada ya kuona ukanda wa Afrika Mashariki ikichezwa michuano ya club Bingwa Afrika Mashariki ikikutanisha timu mbali mbali wakati wa michuano kuendelea Ayo TV imempata katibu mkuu wa CECAFA Nicholaos Musonye.
.
“Simba na Yanga sio wenye CECAFA wanaweza kwenda kucheza wapi lakini Mashindano ya yataendelea bila Yanga na Simba, sisi hatuwezi kukosa timu za maana kucheza CECAFA Yanga na Simba wanafanya nini Afrika? wangekuja kufanya maandalizi”>>> Nicholaos Musonye
,
Mara nyingi imeozeleka kuwa wakati wa michuano ya fainali za timu za taifa kuna kuwa hakuna mashindano yoyote ya ngazi ya vilabu, lengo likiwa ni kupisha michuano hiyo ila chama cha soka Afrika Mashariki na kati CECAFA hawakufanya hivyo na kuendeleza michuano ya Kagame Cup, kitu ambacho kimedaiwa na baadhi ya watu kupoteza mvuto wa mashindano hayo.

VIDEO: Mtangazaji wa Ennahar TV amwaga machozi Algeria ikitinga nusu fainali AFCON

Soma na hizi

Tupia Comments