Habari za Mastaa

Tatizo la kiafya la Justin Bieber lafanya ndoa yake na Hailey kuahirishwa tena

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ unaripoti kuwa ndoa ya mwanamuziki Justin Bieber na mpenzi wake Hailey Baldwin iliyopangwa kufungwa March 25,2019 ambayo ni siku ya kuzaliwa ya Justin Bieber imeahirishwa tena na kuripotiwa kusogezwa mbele.

Huku sababu kubwa ikitajwa kuwa hali ya kiafya ya Justin Bieber kwa sasa sio nzuri, ambapo wiki iliyopita Justin aliandika kuwa ana tatizo la afya kupitia ukurasa wake wa instagram na kuwataka watu wazidi kumuombea. Inaelezwa waalikwa ambao walikuwa wamepokea kadi zao za mwaliko tayari wametumiwa jumbe za kuwaomba radhi.

Inaelezwa kuwa hii ni mara ya nne sasa kwa Justin Bieber na mpenzi wake Hailey Baldwin kuhairisha ndoa yao kwa kutaja sababu mbalimbali.

VIDEO: BIFU!! AMBER LULU NA HAITHAM WATIBUANA, ADAIWA KUIBA MUME

Soma na hizi

Tupia Comments