Michezo

Alex Iwobi kataja sababu za kuamua kuondoka Arsenal na kwenda Everton

on

Staa wa Nigeria na club ya Everton Alex Iwobi ameeleza sababu ya kuamua kuondoka Arsenal katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili na kuijiunga na club ya Everton ya jijini Liverpool.

Iwobi mwenye umri wa miaka 23 ametumia takribani maisha yake yote ya soka katika club ya Arsenal, akiwa kaanzia katika soka la vijaja, huku msimu uliopita ukiwa ni msimu wa mafanikio kwa upande wake akifanikiwa kucheza michezo jumla ya 51 ya mashindano yote.

Katika michezo hiyo akifunga magoli 6 na kutoa assis tisa, kitu ambacho kinadaiwa kuishawishi Everton kutoa pound milioni 35 kumnunua, Iwobi akiwa anasubiri kucheza game yake ya kwanza na Everton ameelezea kilichompelekea kuhama Arsenal.

“Ofa ilikuwa ya kuvutia kiasi kwamba ni ngumu kwa mimi kuikataa, meneja aliniambia kuna nafasi kwa ajili yako na tutakujali, kimsingi aliniambia vitu vyote ambavyo utahitaji kusikia kama mchezaji, amenifanya nijiamini kuwa nitafanya vizuri”>>>Iwobi

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments